1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuatemala

Rais mteule wa Guatemala aapa kuchukua mamlaka Januari

9 Desemba 2023

Bernardo Arevalo amekashifu ombi la ofisi ya mwendesha mashitaka kubatilisha ushindi wake katika uchaguzi wa marudio wa Agosti, akitaja madai ya ukiukwaji wa sheria kuwa "potofu" na "jaribio la mapinduzi."

https://p.dw.com/p/4ZxrO
Rais mteule wa Guatemala Bernardo Arevalo
Rais mteule wa Guatemala Bernardo ArevaloPicha: Cristina Chiquin/REUTERS

Tangu aliposhinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi mnamo Juni, Arevalo na chama chake cha ''Seed Movement'' wamekuwa wakikabiliwa na mfululizo wa uchunguzi kutoka kwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ambayo inadai kuna makosa katika usajili wa chama miaka kadhaa iliyopita.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Arevalo ameapa kuchukua mamlaka ya uraisi kama ilivyoratibiwa Januari 14.

Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimemuunga mkono Arevalo, wakisema uchunguzi huo ni juhudi zilizoratibiwa za kumdhoofisha Arevalo na demokrasia ya Guatemala, nchi yenye watu wengi zaidi Amerika ya Kati.

Hata hivyo Mkuu wa mahakama ya juu ya uchaguzi ya Guatemala Blanca Alfaro, amesema kwamba uchaguzi hautarudiwa.