1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuatemala

Mwendesha mashitaka wa Guatemala abatilisha ushindi wa urais

9 Desemba 2023

Ofisi ya mwendesha mashitaka ya Guatemala imesema uchaguzi uliompa ushindi mgombea Bernardo Arevalo ulikuwa batili, hatua iliyopingwa vikali na washirika wa kikanda wakiita ni jaribio la mapinduzi.

https://p.dw.com/p/4ZxlH
Ofisi ya mwendesha mashitaka ya Guatemala imesema uchaguzi uliompa ushindi mgombea Bernardo Arevalo ulikuwa batili
Ofisi ya mwendesha mashitaka ya Guatemala imesema uchaguzi uliompa ushindi mgombea Bernardo Arevalo ulikuwa batili.Picha: Fernando Chuy/ZUMA Press/picture alliance

Mwendesha mashitaka Leonor Morales amesema jana kwamba uchaguzi huo ulikuwa batili kutokana na makosa yaliyofanyika wakati wa kuhesabu kura.

Arevalo aliyetarajiwa kuingia madarakani Januari 14 amekabiliwa na vizingiti vya kisheria tangu ushindi wake wa kushtukiza katika duru ya pili ya uchaguzi mwezi Agosti, ikiwa ni pamoja na majaribio ya kukisimamisha chama chake na kumzuia kuingia madarakani.

Sekretarieti ya Ushirikiano wa Mataifa ya Amerika, OAS imelaani hatua hiyo iliyosema ni mapinduzi yaliyofanywa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa Guatemala.