1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEcuador

Rais mteule wa Ecuador Daniel Noboa kuapishwa leo

23 Novemba 2023

Mfanyabiashara na milionea Daniel Noboa ataapishwa madarakani nchini Ecuador hii leo baada ya kushinda uchaguzi wa rais wa duru ya pili mnamo mwezi Oktoba.

https://p.dw.com/p/4ZN0Z
Ecuadors gewählter Präsident Daniel Noboa
Daniel Noboa ambae ni mshindi wa kiti cha urais wa EcuadorPicha: Dolores Ochoa/AP Photo/picture alliance

Noboa mwenye umri wa miaka 35 aliyeshinda urais kutokana na ahadi ya kurudisha usalama na kutengeneza nafasi za ajira kwa wananchi wa taifa hilo la Amerika ya Kusini anakabiliwa na changamoto ya kurekebisha hali ya kiuchumi pamoja na kupambana na ongezeko la machafuko yanayosababishwa na magenge ya biashara haramu ya madawa ya kulevya. Ecuador imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya kiuchumu tangu lilipozuka janga la virusi vya Corona na kusababisha maelfu ya raia kuikimbia nchi hiyo. Noboa ataiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miezi 17 tu, kumaliza muhula ulioachwa na mtangulizi wake rais Guillermo Lasso aliyelivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema kuepuka kupigiwa kura ya kuondolewa madarakani.