1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Tshisekedi aapishwa kwa muhula wa pili madarakani

20 Januari 2024

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi ameapishwa kwa muhula wa pili wa miaka mitano baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi uliogubikwa na visa vya udanganyifu.

https://p.dw.com/p/4bV7Z
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix TshisekediPicha: AFP

Felix Tshisekedi alikula kiapo katika uwanja wa michezo wa mashujaa wa uhuru ulioko mji mkuu Kinshasa.

Viongozi wa serikali, wakuu wa nchi za Afrika, na wajumbe wa kigeni kutoka Marekani, China na Ufaransa pia wamehudhuria hafla hiyo.

Kuapishwa kwake kwa mara ya kwanza kulifanyika mnamo Januari 2019 katika bustani ya Ikulu ya Taifa, baada ya ushindi wa utata dhidi ya Martin Fayulu. Bustani hiyo imekuwa ikitumika kuandaa hafla mbalimbali za serikali.

Mnamo Disemba 20, Wakongomani walipiga kura kumchagua rais, wabunge, magavana wa mikoa pamoja na madiwani.