1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Biden asitisha kampeni baada ya kugundulika na UVIKO

18 Julai 2024

Ikulu ya Marekani White House imesema rais wa taifa hilo, Joe Biden amegundulika kuwa na virusi vya UVIKO-19 na kuonesha dalili za kawaida za maambukizi hayo.

https://p.dw.com/p/4iRY0
Uchaguzi wa Marekani 2024 Joe Biden alipimwa na kukutwa na UVIKO
Rais Joe Biden akitembea ili kupanda Air Force One katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harry Reid huko Las Vegas, Julai 17, 2024.Picha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa White House, Karine Jean-Pierre amesema Biden aliyekuwa tayari amepata chanjo dhidi ya virusi vya UVIKO na kadhalika ile ya kuongezewa nguvu alijihisi vibaya baada ya kupata maambukizi hayo.

Hali hiyo ilimfika kiongozi huyo, akiwa kwenye kampeni za uchaguzi huko Nevada. Alikutana na wafuasi mapema Jumatano lakini alikatisha hotuba yake katika jimbo hilo ambalo lina nguvu sawa za ushawishi kati ya chama chake cha Democrats na kile cha Republican.

Hata hivyo Ikulu ya Marekani imesema Biden atarejea katika makazi yake ya kibinafsi huko Delaware ambapo atajitenga huku akiendelea kutekeleza majukumu yake yote kikamilifu wakati huo.