1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Uzbekistan wapiga kura kurefusha utawala wa rais

Sylvia Mwehozi
9 Julai 2023

Raia wa Uzbekistan wamepiga kura siku ya Jumapili katika uchaguzi wa rais ambapo Rais Shavkat Mirziyoyev anawania kurefusha utawala wake kwa muhula mwinginé wa mika saba.

https://p.dw.com/p/4Tdjp
Uzbekistan | uchaguzi wa rais
Raia wa Uzbekistan wakishiriki uchaguzi Julai 9Picha: Vladimir Smirnov/TASS/dpa/picture alliance

Raia wa Uzbekistan wamepiga kura leo Jumapili katika uchaguzi wa rais ambapo Rais Shavkat Mirziyoyev anawania kurefusha utawala wake kwa muhula mwinginé wa mika saba. Uchaguzi huo umefanyika ikiwa ni miezi kadhaa baada ya rais huyo kubadili Katiba ili kuongeza ukomo wa utawala, ambapo kabla ulitakiwa kukamilika mwaka 2026.

Awali, Mirzi-yoyev aliendesha kura ya maoni mnamo mwezi Aprili ya marekebisho ya katiba ambayo iliongeza mihula ya urais kutoka miaka mitano hadi miaka saba. Hata hivyo bado hakuna vyama vya upinzani vyenye nguvu au wanasiasa wanaotarajiwa kuleta ushindani kwa kiongozi hiyo katika uchaguzi wa Jumapili.Uzbekistan yaahidi kuisaidia Marekani kuchunguza ugaidi

Kama mataifa mengine ya Asia ya kati, Uzbekistan inajaribu kupunguza athari za vikwazo vya nchi za Magharibi vilivyowekwa dhidi ya mshirika wake wa jadi wa kibiashara Urusi, kufuatia vita vya Ukraine.