1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uzebkistan yapitisha mabadiliko yakurefusha utawala wa rais

1 Mei 2023

Uzbekistan imeidhinisha mabadiliko ya katiba yatakayompelekea Rais Shavkat Mirziyoyev kusalia madarakani hadi mwaka 2040, katika kura ya maoni iliyokosolewa na waangalizi wa kimataifa kama iliyokuwa na mapungufu.

https://p.dw.com/p/4QkqG
Frankreich Paris | Präsident Usbekistan | Schawkat Mirsijojew
Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Kulingana na matokeo ya awali yaliyotolewa leo, zaidi ya asilimia 90 ya wapiga kura wameidhinisha mabadiliko hayo huku asilimia 85 ya wapiga kura wakijitokeza kushiriki zoezi la upigaji kura hapo jana Jumapili.

Waangalizi kutoka Shirika la Usalama na Ushirikiano la Ulaya OSCE lakini wanasema kura hiyo haikushirikishwa upinzani wa aina yoyote na haikumuwakilisha kila mmoja.

Mirziyoyev mwenye umri wa miaka 65, alichukua uongozi mwaka 2016 baada ya kifo cha dikteta Islam Karimov na amesisitiza kwamba mabadiliko hayo yataboresha utawala na maisha.