1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Matamshi ya Blinken kuhusu Pyongyang na Urusi yakosolewa

11 Novemba 2023

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Korea Kaskazini imeyakosoa matamshi ya mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Antony Blinken aliyetahadharisha juu ya mahusiano yanayotanuka kati ya Urusi na serikali mjini Pyongyang.

https://p.dw.com/p/4Yh9D
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony Blinken na mwenzake wa Korea Kusini Park Jin mjini Seoul.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony Blinken na mwenzake wa Korea Kusini Park Jin mjini Seoul.Picha: Jonathan Ernst/AP Photo/picture alliance

Blinken alitoa matamshi hayo alipokuwa ziarani nchini Korea Kusini mapema wiki hii ambapo alisema ushirikiano wa kijeshi kati ya Moscow na Korea Kaskazini "unaimarika na kuwa hatari" na akairaia China, iliyo mshirika wa karibu wa Pyongyang kutumia ushawishi wake kuidhibiti dola hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Korea Kaskazini imesema matamshi hayo yanazidisha hali ya wasiwasi kwenye rasi ya Korea na kanda nzima na kuitaka Washington "ijifunze kuzoea uhalisia mpya wa uhusiano kati ya Urusi na Korea Kaskazini".

Mataifa ya magharibi na washirika wake yanatiwa mashaka na kujongeleana kwa nchi hizo mbili zilizo chini ya vikwazo vya kimataifa na zenye uwezo mkubwa wa kijeshi.