1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken airai China kuidhibiti Korea Kaskazini

9 Novemba 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken aliye ziarani nchini Korea Kusini ameirai China kutumia ushawishi wake kuidhibiti Korea Kaskazini kuachana na kile amekitija kuwa matendo "yanayoteteresha uthabiti."

https://p.dw.com/p/4Ybot
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Jonathan Ernst/Reuters/AP/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken aliye ziarani nchini Korea Kusini ameirai China kutumia ushawishi wake kuidhibiti Korea Kaskazini kuachana na kile amekitija kuwa matendo "yanayoteteresha uthabiti" kwenye rasi ya Korea ikiwemo mradi tata wa makombora ya masafa unaotekelezwa na utawala mjini Pyongyang.

Blinken ameyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Seoul akiwa pamoja na mwenzake wa Korea Kusini Park Jin.

Zaidi kuhusu mwito wake kwa China Blinken amesema, "China ina uhusiano wa kipekee na Korea Kaskazini. Kutokana na uhusiano huo imekuwa na ushawishi mkubwa na tunatamani China itumie ushawishi huo kubeba dhima yenye manufaa kwa kuhakikisha Korea Kaskazini  inaachana na tabia yake hatari"

Kwenye ziara hiyo iliyojumuisha pia mkutano kati yake na rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini, mwanadiplomasia huyo wa Marekani amezungumzia pia wasiwasi unaongezeka kufuatia kutanuka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Korea Kaskazini.