1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Korea Kaskazini kurudi kwenye meza ya mazungumzo kuhusu silaha za Nuclear

23 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFbV

Katika kile kinachoonekana kuwa kizungumkuti nchini Korea Kaskakazini, kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong amesema yupo tayari kurudia upya mazungumzo juu ya mpango wake wa silaha za nuklear iwapo masharti kadha yatafikiwa.

Kim amenukuliwa akimwambia mjumbe wa china aliyemtembelea kwamba mazungumzo hayo huenda yakarudiwa wakati wowote iwapo Marekani itaonyesha uaminifu na uwazi.

Korea Kaskazini imekubali wazi kwa mara ya kwanza mapema mwezi huu kwamba inamiliki silaha za nuklear lakini ikakataa kurudi kwenye mazungumzo na Marekani,Korea Kusini,China Japan Na Russia.