1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin ashambulia mataifa ya Magharibi kwa kuchochea migogoro

15 Agosti 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin leo ameufungua mkutano wa kimataifa wa masuala ya usalama mjini Moscow na kutumia hotuba yake kuyashambulia mataifa ya magharibi akiyatuhumu kwa kuchochea mizozo na machafuko duniani

https://p.dw.com/p/4VCkf
Russland | Moskauer Konferenz über internationale Sicherheit 2023
Picha: Artyom Geodakyan/dpa/TASS/picture alliance

Katika ujumbe aloutoa kwa njia ya video, Putin amesema sehemu kubwa ya mizozo duniani ni matokeo ya uchu wa kusaka ushawishi, tabia za kibinafsi na ukoloni mamboleo wa mataifa ya magharibi.

Soma pia: Moscow haikatai kuzungumza na Kyiv

"Tunaweza kuona wazi kabisa jinsi sera ya kuongeza mafuta kwenye moto inavyoweza kuleta maafa mfano ukiwa Ukraine. Kwa kuupatia mabilioni ya dola utawala wa manazi mamboleo, kuisambazia silaha, kutuma washauri wa kijeshi na mamluki, kila kitu kimefanywa kuuchochea mzozo huo kuzidi makali na kuyaingiza na mataifa mengine"

Kwenye mkutano huo unaohudhuriwa na karibu wawakilishi 800 kutoka mataifa 76 duniani , Putin amesema lengo la matendo ya mataifa ya magharibi ni kusababisha mizozo na kisha kukwapua rasilimali kwenye mataifa yaliyopoteza utulivu.