1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Moscow haikatai kuzungumza na Kyiv

30 Julai 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Moscow haipingi kufanya mazungumzo na Ukraine kuhusiana na namna ya kuumaliza mzozo baina yao.

https://p.dw.com/p/4UYTh
Afrika-Russland-Gipfel
Picha: Mikhail Metzel/TASS/IMAGO

Akizungumza siku moja baada ya kumalizika kwa mkutano wa kilele na viongozi wa Afrika, raid Vladimir Putin amesema mkakati wa amani wa Afrika unaweza kutumika kama msingi wa amani, pamoja na ule uliowasilishwa awali na China.

Hata hivyo, amesema ni vigumu kufanyika kwa mazungumzo hayo, wakati Kyiv ikiendeleza mashambulizi.

Aidha taarifa nyingine zinasema Saudi Arabia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya kusaka suluhu ya amani yatakayofanyika mwishoni mwa wiki ijayo huko Jeddah.

Vyombo kadhaa vya habari vimesema wajumbe kutoka Ukraine, mataifa ya magharibi na mengine yanayoendelea watahudhuria, lakini Urusi haitashiriki.