1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Prosper Bazombaza aidhinishwa umakamo wa rais Burundi

23 Juni 2020

Bunge la taifa Burundi limemuidhisha Prosper Bazombaza kuwa makamu wa rais Huku Alain Guillaume Bunyoni aliekuwa waziri wa usalama akiidhinishwa kuwa waziri mkuu.

https://p.dw.com/p/3eE8j
Burundi Vereidigung Präsident Evariste Ndayishimiye
Picha: Reuters/E. Ngendakumana

Spika wa Bunge Pascal Nyabenda amesema uteuzi na udhinishwaji wa maafisa hao umelingana na katiba mpya iliopitishwa katika kura ya maoni mwaka 2018.

Pascal Nyabenda spika wa bunge la taifa akitangaza kuidhinishwa Prosper Bazombaza kwenye wadhifa wa waziri mkuu na Alain Guillaume Bunyoni kama waziri mkuu. Kulingana na spika wa Bunge majina ya maafisa hao wawili yalipendekezwa na kufikishwa bungeni na rais Evariste Ndayishimiye na bunge kujumuisha kwenye agenda ya kikao kinacho endelea kabla ya bunge liliyopo muda wake kufikia ukingoni.

Wameidhinishwa na wabunge 92 kati ya 94.

Burundi Vereidigung Präsident Evariste Ndayishimiye
Majenerali wa jeshi la Burundi katika hafla ya kiapo cha raisPicha: Reuters/E. Ngendakumana

Baada ya wabunge kutathimini wasifu wao, maafisa hao wameidhinishwa na wabunge 92 kati jumla ya 94 waloudhuria kikao hicho bungeni huku wabunge wawili wakiwakata, ambapo kulingana sheria ya ndani ya bunge, bunge linaundwa na wabunge 121, wingi unao takikana ili kuidhinisha ama kupitisha maamuzi ni wabunge 61.

Terence Nimubona mbunge kutokana chama CNL cha upinzani kinachoongozwa na Agathon Rwasa amesema udhinishwaji maafisa hao umefanyika kinyume cha sheria. Na kwamba ni swala ambalo halikuwepo kwenye agenda ya bunge jumanne hii.

Soma zaidi: Rais Ndayishimiye ana jukumu la kuleta mageuzi Burundi

Pasacal Nyabinda spika wa bunge, amesema kwa upande wake kuwa hakuna sheria ilokiukwa, na kwamba rais Evariste Ndayishimiye aliekula kiapo tarehe 18 mwezi huu anatakiwa kufanya kazi na Makam mmoja wa rais na waziri mkuu kama inavyo agiza katiba mpya.

Prosper bazombanza alieidhinishwa kuwa Makamu wa rais ni kutoka jamii ya watutsi na tayari alihudumu kwenye wadhifa huo tangu mwaka 2010 hadi 2015. Naye Alain Guillaume Bunyoni alieidhinishwa kuwa waziri mkuu anakalia kiti cha waziri wa usalama na kukabiliana na majanga tangu 2015 hadi wakati huu. Ni kutoka CNDD/FDD tangu ilipokuwa magunguni. Uteuzi wa maafisa hao umekuja wakati uvumi umetanda kwenye mitandao ya kijamii kuwa Hussein Radjabu zamani mkuu wa Chama CNDD/FDD pia atarudi nchini kushirikiana na serikali ya Evariste Ndayishimiye.

Hayo yanajiri wakati serikali imetangaza kuwa mazishi ya rais wa Zamani Pierre Nkurunziza yatafanyika Ijumaa hii katika mkoa wa Gitega, alioteuwa kuwa mji mkuu wa kisiasa.