1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Moscow yawakamata kwa muda wanaharakati wa haki za "mashoga" kutoka Umoja wa ulaya

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxh

Moscow:

Mbunge wa chama cha walinzi wa mazingira cha Ujerumani Volker Beck alikamatwa kwa muda katika mji mkuu wa Urusi Moscow,alipojaribu pamoja na wabunge wengine wa Umoja wa ulaya kushiriki katika maandamano yaliyopigwa marufuku kuwaunga mkono mashoga nchini Urusi.Walikamatwa walipokua wakiandamana nje ya ofisi ya meya na kushambuliwa na wafuasi wa siasa kali za kizalendo.Volker Beck alishiriki hapo awali katika mkutano kuhusu haki za mashoga.Mbali na mbunge huyo wa chama cha kijani-Die Grüne cha Ujerumani , mwanaharakati mwengine mashuhuri wa haki za mashoka kutoka Uengereza Peter Tatchell ni miongoni mwa waliokamatwa pia. Wafuasi kadhaa wa siasa za kizalendo ,wakomonisti na makundi ya kidini waliingilia kati na kuanza kuwapiga ngumi na mateke waandamanaji hao kabla ya polisi kuingilia kati na kuzitawanya pande hizo mbili.