1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Bangladesh wakabiliana na waandamanaji

Sylvia Mwehozi
29 Julai 2023

Polisi wa Bangladesh wamefyatua risasi za mpira na mabomu ya kutoa machozi, kuutawanya umati wa waandamanaji ambao walikuwa wanazuia barabara muhimu katika mji mkuu wa Dhaka,

https://p.dw.com/p/4UXZF
Bangladesh, Dhaka
Waandamanaji mjini DhakaPicha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Polisi wa Bangladesh wamefyatua risasi za mpira na mabomu ya kutoa machozi, kuutawanya umati wa waandamanaji ambao walikuwa wanazuia barabara muhimu katika mji mkuu wa Dhaka, katika maandamano ya hivi karibuni ya kumtaka kiongozi wa nchi kujiuzulu.

Chama cha upinzani cha Bangladesh Nationalist BNP na washirika wake, wameitisha mkururo wa maandamano tangu mwaka jana, yanayomtaka waziri mkuu Sheikh Hasina kuachia mamlaka na kuruhusu kuandaliwa kwa uchaguzi mnamo mwezi Januari.

Ghasia zimezuka katika maeneo kadhaa wakati polisi walipojaribu kutawanya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika tangu mapema asubuhi na kuzuia barabara muhimu. Maandamano ya leo Jumamosi yametatiza usafiri baina ya mji mkuu na maeneo mengine ya nchi. Serikali za magharibi zimeelezea wasiwasi juu ya hali ya kisiasa nchini humo, ambako chama tawala cha Hasina kinadhibiti bunge.