1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Waandamanaji wamtaka waziri mkuu ajiuzulu Bangladesh

11 Januari 2023

Umati mkubwa wa waandamanaji wamejitokeza barabarani katika miji ya Bangladesh leo kumtaka waziri mkuu wa nchi hiyo Sheikh Hasina ajiuzulu.

https://p.dw.com/p/4M253
Bangladesch Ausschreitungen BNP Dhaka
Picha: Mortuza Rashed/DW

Waandamanaji hao vile vile wanataka kuandaliwe uchaguzi mpya, huku ghadhabu ya umma ikiongezeka kutokana na kupanda kwa bei za vyakula na nishati.

Washirika wa upinzani wamefanya maandamano katika mji mkuu Dhaka na miji mingine tisa.

Watu kadhaa wamejeruhiwa katika mji wa katikati mwa nchi wa Faridpur wakati wafuasi wa chama tawala Awami League walipowashambulia waandamanaji huku wakiwa na vijiti na kurusha vilipuzi.

Kiongozi mwandamizi wa chama cha Bangladesh Nationalist, BNP, Mirza Abbas aliyeachiwa kutoka gerezani siku ya Jumatatu amesema nje ya makao makuu ya chama mjini Dhaka kwamba wakati wa kuendelea kubakia madarakani kwa nguvu umefika kikomo na ametaka serikali isiyoegemea upande wowote iandae uchaguzi.

Polisi wanakadiria watu wapatao 50,000 wamehudhuria maandamano ya mjini Dhaka.