1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS;waazimia kuwalinda watoto dhidi ya kuandikishwa kazi ya uanajeshi

7 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUQ

Wajumbe kutoka nchi 58 waliokutana mjini Paris wamekubaliana juu ya kuchukua hatua thabiti ili kuwalinda watoto dhidi ya kutumikishwa kama askari.

Umoja wa Mataifa umesema mwaka jana pekee watoto wapatao laki mbili na nusu chini ya umri wa miaka 19 waliandikishwa kazi ya uanajeshi katika nchi 12 ikiwa pamoja na Sudan,Sri Lanka,Burma na Philippines.