1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Ghasia zaendelea katika miji ya Ufaransa

13 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJ0

Hakuna dalili kuwa ghasia na fujo za kuchoma moto mali zimekomeshwa nchini Ufaransa.Ripoti zinasema wafanya ghasia wamepambana na polisi kati kati ya mji wa Lyon na sehemu zingine.Magari pia yametiwa moto.Polisi wa kuzuia fujo walitumia gesi ya kutoa machozi kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukirusha mawe.Katika mji mkuu Paris polisi kwa maelfu wanapiga doria ili kuzuia mashambulio yanayokhofiwa kutokea katika vituo muhimu kama vile Mnara wa Eiffel.Mikutano yote ya hadhara imepigwa marufuku mpaka jumapili asubuhi,baada ya wito wa kufanya ghasia zaidi,kugunduliwa kwenye mtandao wa Internet na simu za mkononi.Mwisho wa juma katika miji 10 kusini-mashariki mwa Ufaransa,vijana wamekatazwa kutoka nje bila ya kufuatana na watu wazima kati ya saa nne usiku na saa kumi na mbili asubuhi.