1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Wafaransa wataidhinisha katiba mpya ya Umoja wa Ulaya?

28 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF9K

Uchunguzi wa maoni huonyesha kuwa wapiga kura nchini Ufaransa,huenda wakaikataa katiba mpya ya Umoja wa Ulaya,katika kura ya maoni itakayopigwa siku ya Jumapili.Ikiwa Wafaransa watapiga kura kuikataa katiba,basi hatua hiyo itamaanisha mwisho wa mkataba huo.Kabla ya kuweza kuingia kazini,katiba hiyo mpya lazima iidhinishwe na wanachama wote 25 wa Umoja wa Ulaya.Katika kampeni za dakika za mwisho,viongozi wa Ufaransa wamewataka wananchi wenye haki ya kupiga kura waipigie kura Ulaya badala ya kupiga kura ya kuiadhibu serikali ya Ufaransa kuhusika na ukosefu wa ajira unaozidi kuongezeka pamoja na sera zisizopendwa kuhusu soko la ajira.Siku ya Ijumaa,Ujerumani ilikuwa nchi ya tisa katika Umoja wa Ulaya kuidhinisha katiba hiyo.Bunge mjini Berlin lilipiga kura kuiunga mkono katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.