1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Ripoti za gazeti zinasema kuwa Osama bin Laden amefariki.

24 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9X

Ufaransa na Marekani zimesema kuwa haziwezi kuthibitisha ripoti kuwa Osama bin laden amefariki. Gazeti la jimbo moja la Ufaransa linalotolewa kila siku L’Est Republicain limeripoti jana Jumamosi kuwa duru za kijasusi za Saudi Arabia zimeeleza kuwa bin Laden amefariki kutokana na ugonjwa wa typhoid mwezi uliopita nchini Pakistan.

Uchunguzi rasmi umeanzishwa juu ya jinsi nyaraka za siri kutoka katika shirika la kijasusi la Ufaransa zilivyovuja.

Wakati huo huo gazeti la Time limechapisha taarifa katika tovuti yake likielezea duru ambazo hazikutajwa za Saudi Arabia , ambazo zimedai kuwa bin Laden alipatwa na ugonjwa na huenda amekwishakufa.