1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Hatima ya katiba mpya ya Umoja wa Ulaya

29 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF8p

Wafaransa katika kura ya maoni inayopigwa hii leo nchini Ufaransa,wanaamua hatima ya katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa Wafaransa wengi wanaupinga mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya.Ikiwa kweli watapiga kura ya kupinga, basi hiyo humaanisha mwisho wa katiba mpya ya Umoja wa Ulaya,kwani yahitaji kuidhinishwa na wanachama wote 25 wa Umoja huo,kabla ya kuweza kutumika.Lengo la katiba mpya,miongoni mwa mengine ni kurahisisha upitishaji wa maamuzi katika Umoja huo uliopokea wanachama wapya.Kiasi ya Wafaransa milioni 42 wana haki ya kupiga kura na vituo vya kupigia kura vilivyofunguliwa saa mbili asubuhi vitabakia wazi hadi saa mbili usiku.Wakaazi katika miji ya Paris na Lyon wataongezewa muda wa saa mbili zaidi,kupiga kura zao.