1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Ghasia za vijana zaendelea Ufaransa

4 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELy

Polisi nchini Ufaransa kwa usiku wa nane kwa mfululizo wanapambana na machafuko ukingoni mwa mji mkuu Paris.Zaidi ya polisi 1,300 wamesambazwa kupamabana na makundi ya vijana waliohamaki na wanaochoma moto magari na kuharibu majengo.Serikali ya Ufaransa imesema kuwa haitostahamilia machafuko.Ghasia zilianza baada ya vijana wawili wenye asili ya Afrika ya Kaskazini,kufariki kwa ajali ya umeme.Wakaazi wa eneo la ajali hiyo wanaamini kuwa vijana hao walikufa walipokuwa wakifukuzwa na polisi.Lakini ripoti ya polisi wa Kifaransa kuhusu tukio hilo imesema kuwa maafisa walikuwa wakichunguza wizi na hawakuwafukuza vijana hao.