1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis kuwaomba radhi wenyeji wa asili wa Canada

25 Julai 2022

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis yuko nchini Canada ambako anatarajiwa kuomba msamaha kwa wenyeji wa asili ambao ni wahanga wa unyanyasaji uliofanywa kwa muda wa miongo kadhaa katika shule za kikatoliki.

https://p.dw.com/p/4EaK1
Papst zu Besuch in Kanada
Picha: ANSA/ZUMA/picture alliance / ZUMAPRESS.com

Papa Francis aliwasili na kupokelewa na waziri mkuu Justin wa Canada Justin Trudeau pamoja na gavana wa kwanza wa kitaifa wa jamii ya wenyeji wa asili Mary Simon pamoja na viongozi wengine. Ziara ya kiongozi huyo inalenga kuomba msamaha kwa manusura wa unyanyasaji wa kanisa ambao tume ya ukweli na maridhiano ya Canada, imeutaja kuwa "mauaji ya kitamaduni".

Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1800 hadi 1990, serikali ya Canada ilipeleka watoto takribani 150,000 wa jamii ya wenyeji wa asili katika shule za kitaifa zipatazo 139 zilizokuwa zikiendeshwa na kanisa katoliki. Wengi wao walinyanyaswa kimwili na kingono na wakuu wa shule hizo pamoja na walimu. Maelfu ya watoto pia wanaaminika kufariki kwasababu ya magonjwa, utapiamlo au kupuuzwa. Lengo kubwa lilikuwa ni kuwavutia vijana na kuharibu lugha za asilia

Papst Franziskus empfängt Indigene Bevölkerung
Papa Francis akipokea ujumbe wa wenyeji wa asiliPicha: Vatican Media/Catholic Press Photo/IPA/ABACAPRESS/picture alliance

Tangu Mei mwaka 2021, zaidi ya makaburi 1,300ambayo hayakuwa na alama, yaligunduliwa katika maeneo ya zamani ya shule hizo. Ujumbe wa jamii ya wenyeji wa asili, ulisafiri hadi mjini Vatican mnamo mwezi Aprili na kukutana na Papa Francis na baadae aliomba radhi rasmi. Lakini kuomba msamaha kwa mara nyingine ndani ya ardhi ya Canada, kutakuwa na umuhimu mkubwa kwa manusura na familia zao. Mmoja wa viongozi wa wenyeji wa asili RoseAnne Archibald ambaye alikutana na Papa Fracis ametoa raia kwa watu kusimama na wahanga wa unyanyasaji huo.

"Lakini ninataka kuwakumbusha watu kwamba hii inawahusu wale walionusurika, kwamba mchakato huu wote unahusu kuunga mkono na kusimama nyuma ya waathirika wetu na ndiyo sababu tuko hapa leo. Tuko hapa kuwaunga mkono. Na jambo lingine ambalo nilimwambia Papa lilikuwa ni kwamba ninatazamia sana kupita njia hiyo ya uponyaji na kusonga mbele. "

Papa Francis aliwasili katika kiti cha gurudumu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti. Siku ya Jumatatu, atasafiri hadi katika mji ulioko kilometa 100 kusini mwa Edmonton na kuhutubia umati wa watu takribani 15,000 unaotarajiwa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa zamani kutoka kote nchini. Papa Francis ameielezea ziara yake kama "Hija ya toba" na kusema kwamba ana matumaini itasaidia kuponya majeraha ya makosa yote yaliyotendeka. Wakati wa ziara hiyo atakutana na angalau makundi matano ya wenyeji wa asili.Makaburi mengine ya halaiki yagunduliwa Canada

Mbali na kutaka Papa aombe msahama, makundi hayo ya wenyeji wa asili yanashinikiza pia kuruhusiwa kupitia nyaraka za kanisa ili kufahamu hatima ya watoto wao ambao hawakurudi nyumbani kutoka shule za kikataoliki. Wanataka haki pia kwa wahusika wa unyanyasaji, fidia za kifedha na urejeshaji wa vitu vya asili vinavyoshikiliwa na makumbusho za Vatican.