1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asili na mazingiraUmoja wa Falme za Kiarabu

Papa awarai viongozi kupambana na mabadiliko ya tabianchi

3 Desemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo amewahimiza viongozi wa dunia kufanya kazi pamoja kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi

https://p.dw.com/p/4Zio6
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis akiwa Vatican City mnamo Juni 7, 2023
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa FrancisPicha: Ettore Ferrari/ANSA/picture alliance

Papa Franscis ametoa mwito huo katika ujumbe kupitia njia ya video kwa wawakilishi wa kidini wanaohudhuria mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi wa COP28 unaoendelea mjini Dubai. Papa Mtakatifu Francis alishindwa kusafiri kwenye Dubai kutokana na maradhi alaiyoyapata wiki moja iliyopita.

Soma pia: Viongozi wa ulimwengu waanza kuhutubia mkutano wa COP28

Papa Francis amesema wawakilishi wa dini wanapaswa kuwa mfano wa kuonesha inawezekana kubadili mtindo wa maisha na kuwashajihisha viongozi wa kisiasa kuinusuru sayari ya dunia.

Amesema katika ulimwengu wa sasa amani na usalama wa mazingira ndiyo mambo makubwa muhimu na amewataka hasa vijana na watu masikini kuendelea kufanya maombi ili sayari dunia inusurike na athari za kupanda kwa kiwango cha joto.