1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani ya Kusini

Papa Francis alaani mauaji ya mgombea Urais wa Ecuador

12 Agosti 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, leo amelaani mauaji aliyoyataja kuwa ya "kidhalimu" ya mgombea uraisi nchini Equador na kuuurai umma wa taifa hilo kushirikiana ili kudumisha amani.

https://p.dw.com/p/4V68s
Papa Francis
Papa FrancisPicha: Marco Bertorello/AFP

Kiongozi huyo wa kanisa ameyasema hayo kupitia ujumbe wa salamu za rambirambi uliochapichwa kupitia mtandao wa Telegram kufuatia kifo cha Fernando Villavicencio aliyepigwa risasi na kuuwawa wakati wa mkutano wa kisiasa Jumatano wiki hii katika mji mkuu wa Ecuador, Quito.

Soma zaidi: Kifo cha mgombea urais, Ecuador yatangaza hali ya tahadhari

Baba Mtakatifu Francis ambaye aliwahi kuitembelea Ecuador mwaka 2015 amesema anaiombea familia ya Villavicencio na raia wote wa taifa hilo. Tayari watu sita wameshakamatwa kuhusiana na mauaji ya Villavicencio.

Mauaji ya mwanasiasa huyo ambaye alipambana na uhalifu na rushwa katika maisha yake yote yameifanya dunia iitupie jicho nchi hiyo inayoandamwa na wimbi la mauaji yanayotokana na vurugu na uhalifu uliokithiri.