1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis akamilisha ziara yake Ureno kwa kuongoza misa

6 Agosti 2023

Kiongozi wa kanisa Katoliki, Papa Francis, amekamilisha ziara yake ya siku tano nchini Ureno kwa kufanya misa ya Jumapili. Papa alikuwa Lisbon kuhudhuria tamasha la Siku ya Kimataifa ya Vijana wa Kikatoliki

https://p.dw.com/p/4Up3Y
Portugal Papst Franziskus am Fatima Schrein
Picha: Paulo Novais/REUTERS

Kiongozi wa kanisa Katoliki, Papa Francis, amekamilisha ziara yake ya siku tano nchini Ureno kwa kufanya misa ya Jumapili. Misa hiyo inakadiriwa kuwa imedhuriwa na karibu watu milioni 1.5 waliokuwa wameweka kambi katika uwanja mkubwa waliohudhuria hitimisho la siku ya vijana duniani.

Soma pia: Maelfu wajitokeza kumuona Papa nchini Ureno

Katika ibada hiyo iliyofanyika kwenye eneo takatifu la Fatima, Papa hakutoa hotuba bali amezungumza na vijana na kufanya maombi maalumu kwa ajili ya amani ya Ukraine.

Sehemu ya maombi yaliyofanywa na kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani imechapichwa na Vatican katika mtandao wa kijamii wa X uliokuwa ukijulikana kama Twitter hapo awali. Misa hiyo imefanyika mapema ili kuepuka joto kali linalotarajiwa kufika nyuzi joto 40 za Celcius mchana wa leo mjini Lisbon.