1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wajitokeza kumuona Papa nchini Ureno

5 Agosti 2023

Maelfu ya Wakatoliki wamekusanyika mapemahii leo katika eneo takatifu la Fatima nchini Ureno ambako kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis atasali rozali na vijana wagonjwa, watu wenye ulemavu na wafungwa.

https://p.dw.com/p/4Uo6f
Papa Francis akisalimiana na waumini mjini Lisbon
Papa Francis akisalimiana na waumini mjini LisbonPicha: Miguel A. Lopes/AP Photo/picture alliance

 Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki aliwasili katika mji mkuu wa Ureno, Lisbon, mapema Jumatano kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya vijana duniani ambayo vijana wa madhehebu hayo ya Kikristo hukusanyika kila baada ya miaka miwili au mitatu katika mji tofauti.

Ziara hiyo ya Papa Francis inatarajiwa kukamilika kesho Jumapili kwa ibada atakayoiongoza. Ziara ya Papa inaendelea wakati ambapo mamlaka ya hali ya hewa ya Ureno imetangaza tahadhari ya kuwepo kiwango cha juu cha joto mwishoni mwa juma hili mjini Lisbon, kinachotarajiwa kufikia nyuzi joto 41.