1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

pande zinazohasimiana nchini Ivory Coast zimekubaliana kuwavua silaha waasi

15 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFN7

Bouake:

Wawakilishi wa jeshi la Ivory Coast (FANCI) wamekutana na viongozi wa wanamgambo mjini Bouake na kukubaliana juu ya mpango wa kuwavua silaha wanamgambo hao.Mazungumzo yao ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita mjini Pretoria nchini Afrika kusini ambako pande hizo mbili zinazohasimiana ziliahidi kumaliza haraka ugonvi wao,kuwapokonya silaha wanamgambo na kuitisha uchaguzi kama ilivyopangwa mwezi october mwaka huu.Tarehe halisi ya kuanza kuwavua silaha wanamgambo itatangazwa jumamosi ijayo.Mtaalam wa kijeshi wa Afrika kusini,jenerali MXOLISI SHILUBANE aliyehudhuria mkutano huo ,amesifu moyo wa suluhu wa pande hizi mbili.Mkuu wa vikosi vya wanajeshi wa Ivory Coast Major kanali Philippe Mangou,mkuu wa wanamgambo,kanali Sumaila Bakayoko,waziri mkuu Seydou Diarra na mkuu wa tume ya Licorne ya Ufaransa,jenerali Henri Pocet ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo wa Bouake. Mkutano huo umefuatia nasaha ya rais Thabo Mbeki wa Afrika kusini aliyeshauri watetezi wote waruhusiwe kupigania kiti cha rais uchaguzi utakapoitishwa mwezi october ujao.