1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pande hasimu Sudan zakubaliana kusitisha mapigano kwa siku 7

21 Mei 2023

Pande hasimu nchini Sudan, zimekubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba kuanzia Jumatatu. Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani, pande hizo kwa mara ya kwanza zimefanya makubaliano na kutia sahihi zao.

https://p.dw.com/p/4Rcyr
Sudan Khartum Kämpfe Bürgerkrieg
Picha: Mohamed Nureldin/REUTERS

Taarifa iliyotolewa Jumamosi jioni imesema kwamba makubaliano hayo  ya kuweka chini silaha yaliyofanyika mjini Jeddah Saudi Arabia, yanakusudia kuwapa watu wa Sudan nafasi ya kupata misaada ya kiutu.

Mazungumzo ya kusimamisha mapigano kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattahal-Burhan, dhidi ya kikosi cha dharura cha RSF kinachoongozwa na Hamdan Daglo yanasimamiwa na Marekani pamoja na Saudi Arabia.

Mzozo wa kugombea madaraka kati ya jeshi la Sudan na kundi la RSF yameitumbukiza Sudan ndani ya mzozo mkubwa wa kibinadamu uliowalazimisha zaidi ya watu milioni 1.1 kukimbia makwao ikiwemo kuingia kwenye mataifa jirani.