1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshambulizi ya anga yatikisa tena Khartoum na Bahri

20 Mei 2023

Mji mkuu wa Sudan, Khartoum na mji dada wa Bahri imetikiswa tena na mashambulizi ya anga siku ya Ijumaa wakati mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa kikosi maalum cha RSF yakiingia wiki yake ya tano.

https://p.dw.com/p/4RbLa
Sudan Khartum Kämpfe Bürgerkrieg
Picha: Mohamed Nureldin/REUTERS

Mapigano hayo yamezidisha mzozo wa kibinadamukwa watu walionaswa na kukwama ndani pamoja na raia wengine waliokimbia makaazi yao.

Kumekuwa na ripoti za uporaji mkubwa unaofanywa na watu wenye silaha na raia na hivyo kuongeza masaibu kwa wakaazi wa Khartoum. Hapo jana, kiongozi wa kijeshi nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah Burhan alimfuta kazi kiongozi wa kikosi maalum cha wanamgambo cha RSF, ambaye alikuwa mshirika wake wa zamani na aliyegeuka kuwa hasimu wake Mohammed Hamdan Dagalo. Dagalo alikuwa akishikilia nafasi ya naibu kiongozi wa Baraza la uongozi la Sudan.

Inakadiriwa kuwa watu zaidi ya laki 800,000 wamekuwa wakimbizi wa ndani na karibu laki 300,000 wamekimbilia nchi za jirani.