1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Panama yautambua ushindi wa upinzani huko Venezuela

3 Agosti 2024

Nchi ya Panama imetangaza kumtambua mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez Urrutia kama mshindi halali wa uchaguzi wa urais wa Venezuela, na hivyo kutupilia mbali madai ya ushindi ya rais Nicolas Maduro.

https://p.dw.com/p/4j4Ji
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro (kushoto) na mgombea Edmundo Gonzalez Urrutia
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro (kushoto) na mgombea Edmundo Gonzalez UrrutiaPicha: Gustavo Moreno/AP/Pedro R. Mattey/Anadolupicture alliance

Rais Jose Raul Mulino ameandika kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X kwamba Panama inaungana na mataifa mengine kumtambua Gonzalez kama rais aliyechaguliwa wa Venezuela, na kusisitiza kuwa kuheshimu matakwa ya raia ndio msingi wa demokrasia.

Marekani pia ilitangaza wiki hii kumtambua Gonzalez kama mshindi wa uchaguzi huo. Upinzani na wananchi wanapinga matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi na yaliyompa ushindi rais Maduro.

Soma pia: Upinzani Venezuela kuandamana kupinga ushindi wa Maduro

Siku ya Ijumaa, majambazi waliofunika nyuso zao walivamia ofisi za chama cha upinzani, siku moja baada ya kiongozi mkuu wa upinzani Maria Corina Machado kusema anaishi kwa sasa mafichoni akihofia kuhusu uhai wake.