1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Pakistan kumchagua rais mpya

9 Machi 2024

Wabunge nchini Pakistan leo wanatarajiwa kumchagua rais mpya katika kinyang'anyiro kati ya chama tawala cha waziri mkuu Shehbaz Sharif na upinzani unaoongozwa na chama cha waziri mkuu wa zamani Imran Khan aliye gerezani

https://p.dw.com/p/4dKnI
Rais wa Pakistan  Arif Alvi (kulia) akimuapisha waziri mkuu mpya wa nchi hiyo Shehbaz Sharif (kushoto) mnamo Machi 4,2024
Rais wa Pakistan Arif Alvi (kulia) na waziri mkuu mpya wa Pakistan Shehbaz Sharif (kushoto)Picha: Pakistan's President Office/AP/picture alliance

Wagombea wawili wanawania rasmi wadhifa huo wa urais ambapo zaidi ya wabunge 1,000 katika bunge la taifa na mabaraza ya wawakilishi ya majimbo wanatarajiwa kushiriki kura hiyo ya leo.

Wagombea wa urais

Asif Ali Zardari, mgane wa waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto, anagombea nafasi hiyo kwa mara ya pili. Alimaliza muhula wake wa kwanza wa miaka mitano mnamo mwaka 2013.

Soma pia:Wapinzani wa waziri mkuu wa zamani Pakistan Khan kuunda serikali ya muungano

Mahmood Khan Achakzai, mwenyekiti wa chama cha Pashtoonkhwa Milli Awami (PkMAP) kutoka jimbo la Kusini-Magharibi la Balcohistan, anaungwa mkono na chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI).