1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyakakoma, Congo. Watu wenye silaha washambulia vijiji mashariki ya Congo.

17 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtv

Watu 41 wenye silaha pamoja na wanajeshi wawili wa serikali wameuwawa mashariki ya Congo katika mapigano wiki hii kati ya jeshi na wanamgambo wa eneo hilo pamoja waasi wa Kihutu kutoka Rwanda. Msemaji wa jeshi amesema kuwa maelfu kadha ya wapiganaji hao wamekimbia msituni lakini hadi ilipofika Ijumaa jeshi la Congo lilikuwa limekichukua kijiji cha mwisho kati ya vijiji vitatu vilivyochukuliwa na wapiganaji hao karibu na mpaka na Uganda , na kuruhusu raia kurejea katika vijiji vyao ambavyo vilikuwa vimeharibiwa pamoja na mali zao kuibwa.