1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Nigeria yatuma wanajeshi kuwaokoa wanafunzi waliotekwa nyara

9 Machi 2024

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ametuma vikosi vya kijeshi kuwaokoa zaidi ya wanafunzi 250 waliotekwa nyara na watu wenye silaha kutoka shule moja iliyoko Kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4dKnJ
Rais wa Nigeria Bola Tinubu katika mkutano na wafuasi wake katika makao makuu ya chama chake mnamo Machi 1, 2023
Rais wa Nigeria Bola TinubuPicha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Katika taarifa, Rais Tinubu amesema kuwa amepokea maelezo kutoka kwa maafisa wakuu wa usalama kuhusu matukio hayo mawili, na ana imani kwamba waathiriwa wataokolewa.

Maafisa wa serikali wathibitisha kuhusu utekaji nyara

Maafisa wa serikali katika jimbo la Kaduna, wamethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo la utekaji nyarasiku ya Alhamisi, lakini hawakutoa takwimu wakisema kuwa bado wanachunguza idadi ya watoto waliotekwa nyara.

Soma pia: Wanafunzi wasiopungua 287 watekwa nyara kaskazini mwa Nigeria

Matukio hayo ya utekajai nyara, yanaonesha changamoto inayomkabili Tinubu, ambaye aliahidi kuifanya Nigeria kuwa salama na kuvutia uwekezaji zaidi wa kiuchumi kutoka nje.