1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanafunzi 287 watekwa nyara kaskazini mwa Nigeria

Sylvia Mwehozi
8 Machi 2024

Watu wenye silaha waliishambulia shule katika eneo la Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria jana Alhamisi na kuwateka nyara wanafunzi wasiopungua 287.

https://p.dw.com/p/4dI5o
Wanafunzi Nigeria
Wanafunzi wa shule NigeriaPicha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Watu wenye silaha waliishambulia shule katika eneo la Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria jana Alhamisi na kuwateka nyara wanafunzi wasiopungua 287. Huo ni utekaji nyara mkubwa wa pili katika taifa hilo la Afrika Magharibi katika muda wa chini ya wiki moja.

Vyanzo katika eneo hilo, vinasema kwamba washambuliaji waliizingira shule inayomilikiwa na serikali katika mji wa Kuriga ulioko jimbo la Kaduna wakati wanafunzi walipokuwa wanajitayarisha kuanza masomo.

Soma : Wanafunzi 120 hawajulikani walipo baada ya shambulio la shule Nigeria

Hapo awali, mamlaka zilikuwa zimetaja idadi ya wanafunzi waliotekwa kuwa ni zaidi ya 100. Lakini mwalimu mkuu wa shule hiyo Sani Abdullahi alieleza kwamba waliotekwa ni wanafunzi 287.

Utekaji nyara wanafunzi kutoka shule za kaskazini mwa Nigeria umekuwa ni jambo la kawaida na chanzo cha wasiwasi tangu 2014 wakati wanafunzi zaidi ya 200 wa Chibok walipotekwe kwenye jimbo la Borno.