1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger yaliamuru jeshi kuwa kwenye tahadhari kubwa

26 Agosti 2023

Watawala wa kijeshi wa Niger wameliamuru jeshi kuwa katika tahadhari kubwa, wakidai kuna hatari ya uwezekano wa kushambuliwa.

https://p.dw.com/p/4VbuE
Niger | General Abdourahmane Tiani
Picha: Balima Boureima/Reuters

Kiongozi wa ulinzi amesema tahadhari hiyo inaruhusu wanajeshi kujibu mashambulio wakati wowote ili kuepuka mashambulizi ya kushtukiza.

Jumuiya ya kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS imekuwa ikijaribu kujadiliana na viongozi waliofanya mapinduzi Julai 26, lakini imesema iko tayari kutuma wanajeshi wake kurejesha utawala wa kikatiba iwapo juhudi za kidiplomasia zitafeli. 

ECOWAS yakataa kipindi cha mpito cha miaka mitatu Niger

Lakini mkuu wa kamisheni wa Jumuiya hiyo Omar Alieu Touray, hapo jana alisisitiza kuwa ECOWAS haijatangaza vita kwa watu wa Nigerwala hakuna mpango wowote wa kutangaza vita kama inavyodhaniwa kuwa wanataka kuivamia nchi hiyo kijeshi. 

Uamuzi wa jumuiya hiyo mwanzoni mwa mwezi Agosti wa kupeleka wanajeshi wake Niger ulizua hofu ya mzozo kutanuka na kuliyumbisha eneo la Sahel linalopambana na uasi.