1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni Germany na Spain, robo fainali ya EURO 2024

7 Julai 2024

Timu ya taifa ya Ujerumani Die Mannschaft muda mfupi ujao itateremka uwanjani kuvaana na Uhispania katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2024.

https://p.dw.com/p/4hw1D
Euro 2024 | Ujerumani dhidi ya Denmark
Wachezaji wa kikosi cha Ujerumani Antonio Ruduger na Nico Schlotterbeck baada ya mechi kati yao na Denmark kwenye michuano ya EURO 2024Picha: Patrick Scheiber/IMAGO

Nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Ilkay Gündoğan amesema kila mchezo uliobakia mbele yao wanauchukulia kama fainali.

Hii ni robo fainali ya kwanza kwa Ujerumani katika michuano mikubwa ndani ya muda wa miaka minane huku mashabiki wakiwa na matarajio ya kupata ushindi licha ya kupambana na Uhispania ambayo ni moja ya timu bora kwenye michuano hiyo hadi sasa.

Baadaye usiku mjini Hamburg, nyota Cristiano Ronaldo ataiongoza timu yake ya taifa Ureno dhidi ya Ufaransa katika mechi ya pili ya robo fainali.