1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni kwa nini Pyongyang ilidanganya kuhusu jaribio la kombora?

30 Machi 2022

Wachambuzi wamesema Korea Kaskazini ilisema uwongo ilipodai kuwa imefanikiwa kufanya majaribio ya kombora lake lenye nguvu nyingi zaidi la masafa marefu.

https://p.dw.com/p/49Ezp
Nordkorea | Neue interkontinentale ballistische Rakete ICBM
Picha: Yonhap News Agency/picture alliance

Kulingana na wachambuzi, uwongo huo ulikusudia kuupa utawala wa Kim Jong Un uungwaji mkono, baada ya tukio lenyewe kufeli. 

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Korea Kaskazini, liliripoti kuhusu jaribio hilo lililofanywa Machi 24 na kutajwa kuwa la ajabu, la kombora jipya la masafa marefu aina ya Hwasong-17. 

Shirika hilo lilichapisha picha na video za kiongozi wa nchi Kim Jong Un mwenyewe akisimamia jaribio hilo.

Korea Kaskazini yafyatua kombora kuelekea Mashariki

Lakini wachambuzi wametaja masuala yanayokinzana na madai ya Korea Kaskazini. Mashirika ya intelijensia ya Korea Kusini na Marekani vilevile yamesema kombora ambalo Korea Kaskazini ilifanyia jaribio ni Hwangsong-15, ambalo nguvu yake ni chini ikilinganishwa na kombora la masafa marefu ambalo ilifanyia majaribio mwaka 2017.

Je ni kwa nini Korea Kaskazini itoe madai ya uwongo kuhusu majaribio yake? 

Wachambuzi wanahoji kuwa hatua ya Kim Jong Un mwenyewe kuwa mstari wa mbele kwenye tukio hilo, inaashiria propaganda ilikusudiwa kutafuta uungwaji mkono kwa kiongozi huyo mwenyewe.
Wachambuzi wanahoji kuwa hatua ya Kim Jong Un mwenyewe kuwa mstari wa mbele kwenye tukio hilo, inaashiria propaganda ilikusudiwa kutafuta uungwaji mkono kwa kiongozi huyo mwenyewe.Picha: YNA/dpa/picture alliance

Wachambuzi wanasema baada ya jaribio hilo kushindwa na kombora hilo kulipuka katika anga ya Pyongyang, tofauti na walipofanya jaribio halisi la kombora la masafa marefu, Hwasong-17, nchi hiyo ilihitaji propaganda ya ndani kwa dharura. Kuonyesha ufanisi katika mipango yake ya makombora kabla ya maadhimisho muhimu. 

Mchambuzi Yang Moo-jin, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Korea Kaskazini ilitaka kuwaonesha raia wake 'utiifu' kuelekea kile kijulikanacho kama Siku ya Jua, kwa kumuangazia Kim Jong Un kama kiongozi mwenye uwezo mkubwa kijeshi. Alisema hayo akirejelea maadhimisho ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Kim II Sung ya Aprili 15.

"Lakini jaribio hilo, lilishindwa vibaya na zaidi ya mno, ilitendeka mjini Pyongyang, kwa hivyo watu walishuhudia." Amesema Yang na kuongeza kuwa huenda Kim alifikiri alipaswa kufanya jambo kwa haraka ili kuificha aibu hiyo. "Labda ndiyo sababu alidanganya".

Marekani yawawekea vikwazo maafisa wa Korea Kaskazini

Kim Dong-yup, mhadhiri katika chuo kikuu cha Masomo ya Korea Kaskazini amesema, iwe lilikuwa kombora aina ya Hwasong-15 au Hwasong-17, jaribio lililofanyika Machi 24 lilionesha hatua kubwa za ufanisi ambazo Korea Kaskazini imepiga katika mipango yake ya kutengeneza makombora ya masafa marefu.

Kulingana na wachambuzi, hii si mara ya kwanza Korea Kaskazini kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu majaribio yake ya kuunda silaha.
Kulingana na wachambuzi, hii si mara ya kwanza Korea Kaskazini kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu majaribio yake ya kuunda silaha.Picha: Anthony Wallace/AFP/Getty Images

"Bila shaka ni aina ya kombora lililoboreshwa. Kim Jong Un alikuwa akitafuta silaha mbalimbali kwa sababu za ndani wala si dhidi ya Marekani.

Wachambuzi watilia mashaka ukweli wa madai ya Pyongyang

Wachambuzi wamesema mnamo Januari mwaka 2016, ilijaribu kudanganya kuwa jaribio la kurusha kombora kutumia nyambizi lilifaulu, hata ikaghushi picha za video ilhali ni jaribio lililoshindwa.

Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora kwa kutumia nyambizi

Mason Richey, Professor katika chuo kikuu cha Hankuk, amesema inashangaza kuwa Pyongyang ingali inashikilia dhana ya kughushi au kubambanya mambo hadi ufanikiwe.     

Kulingana na Richey, hali ya wachambuzi huru na maafisa wa intelijensia wa Marekani na Korea Kusini kuweza kugundua kwa haraka uwongo huo, inatia mashaka uaminifu wa Korea Kaskazini.

Ameongeza kuwa ikiwa Pyongyang inaweza kusema uwongo kuhusu jambo la wazi kama kombora la masafa marefu, basi wamekuwa wakisema uwongo kuhusu mambo mengine yasiyoonekana. Mfano kuhusu uthabiti wa vichwa vya makombora yao.

 (AFPE)