1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEWYORK:Vikosi vya usalama vya Iraq vyalaumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu

9 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEcp

Umoja wa Mataifa umearifu kwamba suala la haki za binadamu nchini Iraq linaendelea kuzusha hali ya wasiwasi mkubwa katika Umoja huo.

Ripoti iliyotolewa na ujumbe wa Umoja huo nchini Iraq imearifu kwamba vikosi vya usalama vya Iraq vinakiuka haki za binadamu kwa kiasi kikubwa nchini humo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa maiti nyingi zinazopatikana zinaonyesha dalili ya mateso lakbla ya kuwawa.

Mapema wiki hii Umoja wa Mataifa ulilaani mauaji ya watu watatu yaliyotekelezwa na serikali ya Iraq ukiitaka Iraq iondoshe hukumu hiyo ya kifo.

Wakati huo huo waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Collin Powell amesema hotuba yake ya mwaka 2003 kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa ambapo alidai kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein alikuwa na silaha za maangamizi makubwa ameitaja kuwa jambo ambalo hatolisahau maishani mwake.

Wiki kadhaa baada ya uvamizi wa Marekani nchini Iraq wachunguzi wa Marekani walishindwa kudhibitisha kuwepo silaha hizo nchini humo.