1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK:Condolezza Rice azitaka nchi za ulaya kuwaachia wenyewe wa Iraq uamuzi wa hukumu ya kifo dhidi ya Saddam

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvJ

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice amezitaka nchi za Umoja wa Ulaya kutozungumzia maoni yao juu ya kupinga hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein.

Badala yake bibi Rice amesema uamuzi ni juu ya wairaq wenyewe.

Tume ya umoja wa ulaya na nchi kadhaa za Umoja huo zimekosoa hukumu hiyo na kusema kwamba haikubaliki.

Mahakama kuu ya Iraq iliyofadhiliwa na kushauriwa na Marekani ilimkuta na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu kiongozi huyo wa zamani wa Iraq Saddam Hussein katika kesi ya mauaji ya washia 148 wa kijiji cha Dujail huko Iraq mwaka 1982.

Kesi nyingine inayomkabili Saddam Hussein ambayo inahusiana na madai ya mauaji ya kinyama dhidi ya wakurdi katika kile kinachoitwa mauaji ya Anfal inatazamiwa kuendelea hii leo.