1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Umoja wa Mataifa yashinikiza tena waasi wa Rwanda kuondoka Congo

5 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEUz

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana imesikitikia kitendo cha waasi wa Rwanda kushindwa kuondoka Congo kufikia tarehe 18 mwezi wa Septemba tarehe ya mwisho waliotakiwa kufanya hivyo na imewataka wafanye hivyo hivi sasa bila ya kuchelewa zaidi.

Taarifa iliopitsihwa kwa kauli moja na nchi wanachama 15 wa Baraza la Usalama imesema makundi ya kigeni yenye silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yanaendelea kuwa tishio kwa utulivu mashariki mwa nchi hiyo.

Ikilitaja mahsusi kundi la waasi wa Rwanda la FDLR taarifa hiyo imesema Baraza la Usalama inalitaka kundi hilo kutumia fursa hiyo kwa kuendelea kusalimisha silaha na kurudi Rwanda bila ya kuchelewa na bila ya masharti.

Chini ya makubaliano yaliofikiwa mwezi wa Augusti kati ya Congo,Rwanda na Uganda maelfu ya waasi wa Rwanda kadhalika wale wa Uganda waliahidi kuondoka Congo kufikia Ijumaa iliopita.