1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu kukutana na Biden kwa mazungumzo

20 Septemba 2023

Mchambuzi wa mahusiano kati ya Israel na Marekani Eytan Gilboa amesema mazungumzo hayo hayatakuwa mepesi.

https://p.dw.com/p/4WacC
Serikali ya Biden mara kwa mara imezungumzia wasiwasi wake juu ya mpango tata wa Netanyahu wa mageuzi mapana kwenye mfumo wa haki na ni dhahiri suala hilo litazungumziwa.
Serikali ya Biden mara kwa mara imezungumzia wasiwasi wake juu ya mpango tata wa Netanyahu wa mageuzi mapana kwenye mfumo wa haki na ni dhahiri suala hilo litazungumziwa.Picha: Avi Ohayon/picture alliance/ dpa

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anatazamiwa kukutana na Rais Joe Biden wa Marekani Jumatano, katika mazungumzo yatakayowakutanisha viongozi hao wawili kwa mara ya kwanza tangu kiongozi huyo wa Israel alipoingia madarakani mwaka uliopita.

Maandalizi ya mkutano huo yaliyochukua muda refu pamoja na uamuzi wa ikulu ya White House wa kufanya mkutano huo mjini New York badala ya Washington, kwa pamoja vimetafsiriwa na Israeli kama ishara za Marekani za kutofurahishwa na serikali mpya ya Netanyahu ya mrengo mkali wa kulia.

Mchambuzi wa mahusiano kati ya Israel na Marekani Eytan Gilboa amesema mazungumzo haya hayatakuwa mepesi, ingawa White House yenyewe ikikataa kusema chochote hadi sasa kuhusiana na ajenda za Biden kwenye mazungumzo hayo.

Soma pia:

Biden, Herzog wazungumzia mivutano ya Israel katika ikulu ya White House