1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden, Herzog wazungumzia mivutano ya Israel

19 Julai 2023

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Israel Isaac Herzog, wamefanya mazungumzo kuhusiana na mivutano iliyopo juu ya mabadiliko yenye utata ya idara ya mahakama nchini Israel.

https://p.dw.com/p/4U6eo
Israel | Besuch US-Präsident Joe Biden
Picha: JACK GUEZ/AFP

Herzog amesema licha ya maandamano yanayoshuhudiwa nchini Israel kwa sasa kutokana na suala hilo, demokrasia ya nchi yake haijatikiswa na bado iko imara. Baada ya mkutano huo, taarifa kutoka ikulu ya White House imesema, marais hao wawili wamezungumzia haja ya suala hilo kusuluhishwa kwa njia ya makubaliano.

Herzog atarajiwa kulihutubia bunge la Congress

Ziara hiyo ya afisa wa ngazi ya juu nchini Israel huko Marekani, ambayo imejumuisha mkutano pia na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, ilikuwa ni hatua ya Marekani kuonyesha kuiunga mkono Israel kama mwandani wake. Herzog leo anatarajiwa kutoa hotuba katika bunge la Congress.