1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu avunja Baraza lake la vita nchini Israel

17 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelivunja Baraza la Vita la Israel lilio na wanachama sita, katika hatua iliyotarajiwa,baada ya mwenyekiti wake, Benny Gantz kujiondoa katika baraza hilo.

https://p.dw.com/p/4h8VO
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Abir Sultan via REUTERS

Gantz alijiondoa katika baraza hilo, akidai Netanyahu ameshindwa kuwa na mpango maalum juu ya vita vya Gaza.

Netanyahu sasa anatarajiwa kuwa na majadiliano kuhusu vita hivyo na kundi dogo la mawaziri akiwemo waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, na waziri wa masuala ya kimkakati Ron Dermer aliyekuwa katika Baraza hilo.

Soma pia:Mpango wa usitishaji vita Gaza kuamua hatma ya kisiasa ya Netanyahu

Waziri Mkuu huyo wa Israel amekuwa akipata shinikizo kutoka  kwa washirika wake wa chama chenye misimamo mikali ya kidini katika muungano wake kutoka kwa waziri wa fedha Bezalel Smotrich Waziri wa usalama wa kitaifa Itamar Ben-Gvir, waliotaka kujumuishwa katika Baraza la vita la Israel, hatua ambayo ingeleta mvutano na washirika wake wa kimataifa akiwemo Marekani.