1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu asema kuna uwezekano wa kuachiwa mateka wa Gaza

13 Novemba 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonyesha matumaini lakini yenye tahadhari juu ya uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas

https://p.dw.com/p/4Yjyk
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: imago images/Xinhua

Netanyahu amesema kwenye mahojiano na kituo cha utangazaji cha NBC cha nchini Marekani kwamba kuna uwezekano wa kufikiwa makubaliano, lakini akasema hatapenda kuzungumzia kwa kina. 

Umoja wa Mataifa wasema watu wengi wauwawa katika shule unayoisimamia huko Gaza

Amesema ikiwa makubaliano hayo yatafikiwa, itakuwa ni matokeo ya shinikizo la kijeshi, kwa kuwa pengine ndilo linaweza kupelekea kufikiwa kwa makubaliano, na kuongeza kuwa mashambulizi ya kijeshi ya ardhini katika Ukanda wa Gaza ndio yaliyochochea hatua za kuanzisha mazungumzo.