1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Netanyahu apinga kuipa mamlaka ya Palestina udhibiti Gaza

20 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemwambia Rais wa Marekani Joe Biden kwamba, anapinga wazo la kuipa udhibiti mamlaka ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4bV7Q
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Ohad Zwigenberg/AP/dpa/picture alliance

Katika mazungumzo yake na Biden, Netanyahu amesisitiza kuwa baada ya Hamas kuangamizwa, Israel inapaswa kuwa na udhibiti wa Gaza ili kuhakikisha kwamba eneo hilo halitakuwa tishio tena kwa Israel, suala ambalo linakwenda kinyume na matakwa ya mamlaka ya Palestina.

Viongozi hao wawili walizungumza kwa njia ya simu siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza katika muda wa karibu mwezi mmoja huku Biden akieleza kuwa, bado anaamini kuwepo kwa uwezekano wa Netanyahu kukubali kuundwa kwa taifa la Palestina.

Hata hivyo, afisa mkuu wa Hamas Izzat al-Rishq amepuzilia mbali kauli ya Biden juu ya uwezekano wa Israel kukubali kuundwa kwa taifa la Palestina.

Afisa huyo amesema Biden ni mshirika kamili wa mauaji ya Wapalestina na kwamba hawataraji lolote jema kutoka kwake.