1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Ndege zisizokuwa na rubani za Ukraine zaishambulia Urusi

24 Septemba 2023

Shambulio la ndege isiyokuwa na rubani ya Ukraine, limelenga jengo la utawala katikati mwa mji wa Kursk Kusini mwa Urusi. Haya yamesemwa leo na mamlaka katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4WkDS
Russland l Drohnenangriff in Kursk
Picha: Governor of Russia's Kursk Region Roman Starovoit via Telegram/Handout via REUTERS

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, gavana wa eneo hilo  Roman Starovoyt, amesema paa la jengo hilo la utawala liliharibiwa kidogo na kwamba wafanyikazi wa huduma za dharura wanafanya kazi katika eneo la tukio.

Ukraine imelenga miji ya Urusi kwa karibu kila siku katika mashambulizi ya hivi karibuni kutokana na uvamizi wa Urusi nchini humo ambao sasa umedumu kwa miezi 19. Kursk iko umbali wa kilomita 90 kutoka mpaka na Ukraine.

Mwezi uliopita,  shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani ya Ukraine iliharibu kituo cha reli cha Kursk na kusababisha kujeruhiwa kwa watu watano na uharibifu mkubwa.

Ukraine na Urusi zote zinaripoti kuwepo kwa uvamizi wa mara kwa mara wa ndege zisizokuwa na rubani huku Ukraine ikiongeza mashambulizi yanayolenga kudhibiti tena maeneo yanayoshikiliwa na Urusi.