1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya abiria yashika moto ikitua mjini Tokyo

2 Januari 2024

Ndege ya abiria imeshika moto wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Haneda wa Tokyo nchini Japan. Ni kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya kituo cha televisheni cha Japan TBS leo Jumanne.

https://p.dw.com/p/4anBl
Japan| Uwanja wa ndege wa Haneda
Uwanja wa ndege wa Haneda JapanPicha: Morio Taga/dpa/picture alliance

Ndege ya abiria imeshika moto wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Haneda wa Tokyo nchini Japan. Ni kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya kituo cha televisheni cha Japan TBS leo Jumanne.

Picha za video zimeonyesha abiria wakiondoka kwenye ndege hiyo kupitia milango ya dharura huku moto ukizimwa. Ndege ilikuwa imeshika moto kwa sababu zisizojulikana wakati ilipokuwa ikitua.

Mlipuko ulioandamana na moto ulionekana wakati wa kisa hicho. Ndege hiyo iliharibiwa vibaya. Taarifa za hivi karibuni zinaeleza kuwa yumkini abiria karibu mia nne waliokuwa ndani ya ndege hiyo wameokolewa.