1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Nchi zenyeushawishi zatakiwa kusuluhisha mzozo wa Sudan

11 Mei 2023

Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk kwenye kikao maalum kuhusu Sudan.

https://p.dw.com/p/4RDzv
Schweiz, Genf: Volker Türk, UN-Hochkommissar für Menschenrechte
Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Mkuu wa baraza la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turkameyatolea wito mataifa yenye ushawishi barani Afrika kusaidia kumaliza mapigano nchini Sudan na kusema pande zote zimekiuka sheria za kimataifa.

Ameyasema hayo katika kikao maalumu cha dharura cha siku moja kinachoangazia ukiukwaji wa haki nchini humo tangu kulipozuka mapigano mwezi uliopita.

''Baraza la Haki za Kibinadamu limeitisha kikao hiki maalum kuelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya haki na maisha ya watu wa Sudan. Nachukua fursa hii kuzisihi nchi zote zenye ushawishi katika eneo hili kuhimiza, kwa kila namna, utatuzi wa mgogoro huu.'', alisema Turk. 

Kwenye kikao hicho, mataifa ambayo ni pamoja na Uingereza na Marekani yamelaani ukiukwaji unaofanywa na pande zinazohasimiana na kutoa wito wa uchunguzi zaidi pamoja na uwajibikaji.

Balozi wa Sudan kwenye Umoja wa Mataifa aliyeulezea mzozo huo kuwa ni wa ndani, ametoa wito wa Mataifa ya Afrika kusuluhisha mizozo ya Afrika.