1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mkuu wa misaada wa UN yuko Jeddah kwa mazungumzo ya Sudan

Daniel Gakuba
8 Mei 2023

Griffiths awasili nchini Saudi Arabia, kushiriki katika mazungumzo baina ya pande zinazopigana nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4R255
Schweiz UN l Jemen-Geberkonferenz in Genf l Martin Griffiths
Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya ubinadamu, Martin Griffiths aliwasili nchini Saudi Arabia Jumapili, kushiriki katika mazungumzo baina ya pande zinazopigana nchini Sudan.

Kulingana na msemaji wake, lengo la ziara yake ni kushughuikia mambo yanayohusiana na masuala ya kiutu nchini Sudan.

Hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa Griffiths atakuwa na mchango wowote wa moja kwa moja katika mazungumzo yanayofadhiliwa na Saudi Arabia, juu ya uwezekano wa kusitisha mapigano.

Majerali wanaoongoza pande zinazohasimiana nchini Sudan, hawajatoa maelezo ya kutosha juu ya mazungumzo hayo yaliyoanza mjini Jeddah Jumamosi iliyopita.

Makubaliano kadhaa ya kusitisha uhasama yalifikiwa tangu kuzuka kwa mapigano tarehe 15 Aprili nchini Sudan, lakini yaliambulia patupu.

Mwanadiplomasia wa Saudi Arabia amesema mazungumzo ya sasa hayajapiga hatua yoyote.